Nichague Mimi
Tsuma Wesley Robinson
Tsuma Wesley Robinson
Waaah!
Malkia!
Kumbe ni wewe!
Haha... waaaah!
Naezaketi hapa kando yako?
Haha... Asanti sana yaani.
Nafsi yangu inan'ambia unaelekea mjini kama mimi,
Na... kulingana na msongamano wa magari mjini,
Humu ndani tutapakaa masaa mengi,
Sa... badala ya kukaa kipweke mpaka mjini,
Si tuendelee tu na penye tuliachia jana,
Ha-ha, Ama vipi?
Unajua, Malkia,
Tulikutana siku kabla ya juzi,
Juzi yenyewe, Jana, na leo ndo sisi hawa pia,
Kisadfa tu hata bila ya sisi kupangia,
Ha-ha, huoni ni kama kuna kitu Rabbi anajaribu kutuambia,
Kwa upole tena, ni kama anatunong'onezea,
Ha-ha, kuna kelele humu na ndo tusikilizane naomba karibia.
Malkia,
Nichague mimi,
Nichague mimi nipate kujua utamu wa kupendwa,
Nichague mimi nipate kufahamu uzuri wa kudekezwa,
Nichague mimi moyoni uniongezee raha maridhawa,
Sababu hivi sasa kwenye mapenzi nimepagawa,
Na wewe pekee ndo yangu dawa.
Malkia,
Napenda unavyokaa,
Napenda unavyovaa,
Nataka siku moja nimwite ndugu yako shemeji yangu,
Nataka siku moja nikuite mama ya watoto wangu,
Nataka siku moja kukuandikisha kama mmiliki wa mali yangu,
Nataka siku moja kukutambulisha kwa rafiki zangu kama ubavu wangu,
Yule wa pekee aliyenifanya nitake kususia kazi nibaki naye kwangu,
Yule wa pekee aliyenionyesha mapenzi ya kweli na si pwagu,
Ha-ha, sema ndio tu.
Malkia,
Nifanye leo nitake kutembea kwa ulimi,
Nifanye kando na wewe nitake kuwalipia wote hawa nauli,
Kubali yangu kauli,
Nichague mimi.

Wesley Tsuma’s latest short story, “Karakana ya Kheri,” appeared in issue 3 of Kikwetu. He is in his final year at Masinde Muliro University of Science and Technology where he is studying for a bachelor’s degree in journalism and mass communication. He is passionate about a changed society in terms of a society without rape, inequality, corruption, and poverty. Through his articles and poems, he hopes to reach many people and help change society.